Saturday, November 14, 2009

wadau watembelea kijungu na daraja la mungu


daraja la mungu juu ya mto kiwira wilayani rungwe

Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO tulipata nafasi ya kufanya ziara ya mafunzo kwa wenzetu wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Mkoani Mbeya UWASA tarehe 13 – 16 October 2009.
Tulibahatika pia kutembelea sehemu za kitaliii ambazo kwa kweli Wizara ya Maliasili na Utalii ikizitangaza, itakuwa ni sehemu ya kuweza kuliingizia Taifa letu mapato kwa namna Fulani!
Picha ya pili, tatu na nne ni sehemu inayoitwa KIJUNGU, wenyeji wanasema sehemu hii ni ya maajabu makubwa, maji hutumbukia hapo (pamekaa kama chungu) na hayaonekani huelekea wapi! inasemekana mtu akitumbukia eneo hili hawezi kuonekana hadia baada ya siku saba na tena baada ya kufanyiwa mila na wenyeji wa eneo hili.
Sehemu hii inasemekana aliwahi kutumbukia mtu mmoja tu na kutoka akiwa hai! Na alipotoka aliokoka na kuhama sehemu hii kutokana na maajabu aliyoyakuta humo ndani!
Picha ya juu inaonyesha sehemu ya maajabu mengine sehemu hii hii, ni dalaja la ajabu ambalo linavukaa mto Kiwira! Wenyeji wanaliita daraja la Mungu
Mdau Lameck Victor Kashindye
Dawasco HQ


mdau akivinjari daraja la mungu
wadau chini ya daraja la mungu
wadau wakila pozi kwenye 'Kijungu'
juu ya kijungu

1 comment:

  1. Hivi ni baadhi tu ya vivutio mkoani Mbeya ambavyo serikali hii haijaweka mikakati madhubuti ya kuviendeleza. Ni vivutio ambavyo vingeweza kulingizia Taifa hususa mamlaka ya mkoa mapato mengi. Napendekeza kama serikali itashindwa kuviendeleza basi mamlaka ya mkoa ifanye hivyo kwa maslahi ya mkoa na watu wake.

    ReplyDelete