Friday, October 16, 2009

Tunatofautiana Kimwitikio

Mapenzi

Kuna tofauti kubwa sana ya maana na mwitikio wa mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.

Wanaume kawaida wanauwezo wa kutenganisha mwili na moyo(Body and Heart)
Kwa upande wa wanawake tunaweza kusema wao wamekomaa kimapenzi kuliko wanaume kwa sababu kwao kutenganisha mwili na moyo inakuwa vigumu na wakati mwingine haiwezekani.

Mwanamke anapompenda mwanaume huanza na hisia za ndani ya moyo wake then hisia za nje za mwili wake;
wakati mwanaume anapompenda mwanamke huanza kupenda kuanzia hisia za mwilini mwake kwenda then hisia za moyo wake.

Ni rahisi mwanaume kukwambia anakupenda kumbe hakupendi lakini anakutamani tu na wanawake wamekuwa wanaumizwa sana na wanaume kutokana na hii style yao ya kupenda kwa kumuweka mtu moja kwa moja kwenye moyo wake.

Utafiti wingi unaonesha kwamba wanawake wengi huwa hawafurahii kufanya mapenzi na mwanaume asiyempenda;
wakati wanaume wanaweza kufurahia na kupata raha ya mapenzi (kufika kileleni) hata kwa mwanamke asiyempenda.

Ndiyo maana mwanaume anaweza kutembea na mwanamke yeyote hata kama ni mbaya kila idara ukilinganisha na mke wake.
Ndiyo maana matukio mengi ya ubakaji hufanywa na wanaume.

Wanaume wanaweza kutenganisha upendo na kufanya mapenzi (love and sex)
Wanawake hutazama kufanya sex ni kitendo cha ziada baada ya upendo wa kweli na wakati mwingine hufanya mapenzi ili kuimarisha mapenzi kwa mwanaume, wakati wanaume sex ni kwa ajili ya kufurahia tu siyo lazima awe anampenda mwaname anataka kufanya naye sex.

Kwa mwanaume kufanya sex ni kitu kinachofanywa nje ya mwili (out-of-body experience) kwa sababu viungo vyake vya kufanyia sex vipo nje na anapofanya mapenzi anakuwa anafanya kitu kwa mtu mwingine (mwanamke) kama vile kupigilia msumari kwenye ukuta.

Kwa upande wa wanawake viungo vya sex vipo ndani ya mwili na kwao kufanya mapenzi ni kama kumkaribisha mtu ndani ya nafsi yake, hivyo inakuwa ngumu kutenganisha mwili, moyo na hisia zake.

Kama ilivyo kwa watu wote kwamba mtu mgeni akiingia nyumbani kwako hutajisikia raha kwanza au hutajisikia salama hadi ufahamiane, ndivyo wanawake walivyo.
Kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu au mgeni au asiyempenda ni sawa na mtu anayeingilia mipaka ya shamba la mtu, (trespace)

Kumvamia mwanamke bila kuonesha upendo wa kweli ni sawa na kuvamia mipaka ya mashamba ya watu, au ni sawa na kuingia kwenye nyumba za watu bila kukaribishwa.
Hivyo wanawake kwao ni ngumu kutenganisha love na sex

Wanapenda kuwa na ukaribu na mapenzi ya kweli ili kumruhusu mtu kuwa naye kitandani na kuingia kwenye nafasi yake ya siri kufanya mapenzi.
Ndiyo maana huwa wanajisikia kutumiwa na kuumizwa na mwanaume ambaye haoneshi upendo wa kweli.

Wanahitaji mwanaume anayewasililiza, anayewapenda, anayewajali, anayekuwa tayari wakati anamuhitaji, mwanaume anayebembeleza, mwanaume ambaye anajua kuwahudumia wao kama viumbe rasmi na maalumu Mungu ametoa zawadi kwa wanaume duniani.

Swali

Je Mumeo ni mwanaume anayepigilia misumari tu? au ni mwanaume anayeingia kwenye mipaka ya mashamba ya watu? au ni mwanaume anayeingia kwenye nyumba za watu bila kukaribishwa?

Jibu

Jibu unalo wewe kama ni mwanaume una kazi ya kufanya na kama ni mwanamke una kazi pia ya kufanya katika hili.


‘Nawatakia maisha mema’

No comments:

Post a Comment